Rais Samia Ampokea Rais wa Finland, Alexander Stubb, Ikulu Dar
Global Publishers May 14, 2025
SHARE THIS:
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia akiwa na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Finland Alexander Stubb mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Mei, 2025.
Rais wa Finland, Alerander Stubb amewasili nchini Tanzania kwa ziara ya Kitaifa ya siku tatu kuanzia leo Jumatano, Mei 14, 2025.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amempokea mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Finland, Alexander Stubb katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Wakati wa ziara hiyo, viongozi hao watafanya mazungumzo ya ngazi ya juu yanayolenga kuimarisha uhusiano uliopo kati ya Tanzania na Finland.
Nchi zote mbili zimejidhatiti kuimarisha ushirikiano kwa kuongeza mahusiano ya kiuchumi na kuchunguza njia mpya za ushirikiano katika maeneo yenye maslahi ya pamoja.
Rais wa Jamhuri ya Finland Alexander Stubb akikagua Gwaride la heshima lililoandaliwa na Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Mei, 2025.Rais Samia akiwa amesimama na mgeni wake Rais wa Jamhuri ya Finland, Alexander Stubb wakati wimbo wa Taifa wa Tanzania na ule wa Finland ukiimbwa katika viwanja vya Ikulu Jijini Dar es Salaam tarehe 14 Mei, 2025.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia akiwa kwenye picha ya pamoja na Rais wa Jamhuri ya Finland Alexander Stubb, Ikulu Jijini Dar.