×

Wajumbe Wapya Wanne Wachaguliwa Kujiunga na Kamati Kuu ya CCM Taifa

Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), katika kikao chake maalum kilichofanyika Jumatano tarehe 28 Mei 2025, jijini Dodoma, imefanya uchaguzi wa Wajumbe wanne wa Kamati Kuu.

Wajumbe waliochaguliwa kuwa sehemu ya Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa ni:
1. Namelock Edward Sokoine
2. Dkt. Juma Abdallah (Mabodi)
3. Salim Faraj Abri (Asas)
4. Hamad Hassan Chande

Hii ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, CPA. Amos Gabriel Makalla.