×

Internet Society (ISOC) Makao Makuu Yatembelea Miradi Nchini Tanzania

Rais wa ISOC Tanzania Dkt Nazarius Kirama akielekeza jambo kwenye moja ya kituo cha kutoa huduma za Internet kilichopo Shule ya Paul Makonda iliyopo Kigamboni Dar.
Uongozi wa Makao Makuu ya Internet Society kutoka Marekani umetembelea   Tanzania kuangalia shughuli zinazotekelezwa na Chapter ya Tanzania ikiwemo mradi wa Intaneti kwa jamii unafanyika katika Wilaya ya Kigamboni
Wadau katika picha ya pamoja baada ya kukikagua kituo cha Internet kilichopo Shule ya Paul Makonda Kigamboni, Dar.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Rais wa Internet Society Tanzania Chapter Dkt.Nazar Kirama amesema ujio huo ni fursa kwa nchi katika kuendelea  kutanua uwigo wa matumizi ya Internet pamoja na Elimu ya Kidigiti.
Mmoja wa wageni hao akizungumza na wananchi (hawapo pichani).
Kirama amesema  pamoja na ugeni huo wametembelea Chuo Kikuu  Huria  Tanzania (OUT) kutokana na kuwa mfumo wa utoaji wa elimu kwa masafa ya Internet hivyo Internet Society ndio sehemu wanaangalia katika kutumia vituo hivyo katika kuweka internet kwa ajili ya kupeleka internet kwa jamii.
Mmoja wa wakazi wa Kigamboni, Dar akieleza jambo mbele ya ugeni huo.
Katika ziara hiyo wametembelea mradi wa Internet wa Shule ya msingi Ufukoni na Sekondari Paul Makonda   ambao umeunganisha na huduma zingine za kijamii kwa gharama nafuu.
Wadau wakishuhudia mambo yanavyoendelea.
Amesema upatikanaji wa gharama nafuu unatokana idadi ya wanaojiunga kutumia huduma gharama zake zinashuka kwa kiasi kikubwa.
Dkt Kirama na wageni hao wakitafakari jambo.
Hata hivyo amesema kuwa kutokana na Internet Society katika  mikakati walioiweka ni kuhakikisha  kila mtu anapata huduma ya internet bila kikwazo na kwa agharama nafuu.
Dkt.Kirama amesema kuwa  makubaliano na OUT ni fursa kubwa kwa jamii zinazozunguka vituo vyake kupata huduma ya mawasiliano ya Internet.