×

Singida Black Stars Wanawasubiri Yanga fainali Uwanja wa Amaan Zanzibar

HUSSEN Masanza, Ofisa Habari wa Singida Black Stars

HUSSEN Masanza, Ofisa Habari wa Singida Black Stars amesema kuwa wanawasubiri wapinzani wao Yanga SC kwenye fainali ya CRDB Federation Cup ili kufanikisha mpango wao wa kutwaa ubingwa kwa ushindi wa jasho uwanjani.

Yanga SC Juni 9 2025 kupitia kwa Meneja wa Habari Ali Kamwe walibainisha kuwa hawatakuwa tayari kucheza mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Juni 28 2025, Uwanja wa Amaan Zanzibar.

Masanza amesema: “Tunaendelea na maandalizi kwenye mechi zetu mbili ambazo zimebaki kisha baada ya hapo tutaanza kufanya maandalizi kuelekea mchezo wetu wa fainali wa CRDB Federation Cup na tunahitaji ushindi wa jasho.”

Stori na Lunyamadzo Mlyuka, GPL

Wasiliana na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu itazinduliwa rasmi Julai 24 2025 usipange kukosa.