×

EFTA, GSM Kuwakomboa Wafanyabiashara Wadogo na Kati

Mkurugenzi wa GF Vehicles Assemblers (GFA), Ally Jawad Karmali akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda hicho wakati wa sherehe za uundwaji wa gari ya 4000 iiliyotengenezwa katika kiwanda hicho na mafundi wa ndani kutoka vyuo mbalimbali nchini kwa kushirikiana na wataalamu wa kigeni iliyofanyika Kibaha mkoani Pwani.

Taasisi ya kifedha ya EFTA na GSM  zimesaini mkataba wa makubaliano ya kusaidia wafanyabiasha wadogo na kati kukuza biashara zao kupitia mikopo nafuu isiyo na dhamana  ya vifaa ,magari na vitendea kazi ili kujiimarisha kiuchumi ambapo ni muendelezo taasisi hiyo katika kuwafikia wafanyabiashara wengi zaidi nchini, kuwawezesha vifaa kama mashine na magari.

Wafanyakazi wakiwa katika hafla hiyo.

Akizungumza wakati wa kusaini mkataba huo, Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Makampuni ya  GSM,  Benson Mahenya amesema wameamua kushirikiana na EFTA  kutokana na kutambua  umuhimu wa shughuli  za uzalishaji wanazozifanya pamoja na wateja wao.

Mahenya amesema kupitia mkataba huo, mawakala na wadau wanaosambaza bidhaa zao ambao wanakosa mikopo kwa vigezo vya kawaida wataweza kupata mikopo ya magari kutoka EFTA kupitia dhama na yao.

“Naamini kwa kufanya hivi tutagusa maisha ya kila mtu na kuongeza thamani ya biashara wa wadau wetu na kuongeza msaada.”

Ameeleza kuwa kutokana na shughuli nyingi wanazofanya ikiwamo usalishaji wa vinywaji,  pia wamejikita zaidi katika kuimarisha usafirishaji wa matunda kama malighafi ili kuondoa uharibifu.

” Sisi tumeona ni vyema tukaimarisha usafirishaji wa matunda kwa kwenda eneo la uzalishaji ili yasiharibike na kupotea pia kumpa thamani mkulima,” amesema.

Kwa upande wake  Mkuu wa Mauzo na Masoko wa EFTA Tanzania, Clerius Asiel amesema  kwa zaidi ya miaka 20 wamekuwa nguzo muhimu kwa wafanyabiasha wadogo na kati nchini kwa kuwasidia kuwasaidia kumiliki mashine na magari kwa mikopo nafuu bila dhamana.

Ameeleza kuwa mkataba huo na GSM umekuja baada ya kuwezesha upatikanaji wa magari zaidi ya 60 ya kusambaza bidhaa za kampuni hiyo.

” Hatua hii ni kielelezo cha maono yetu ya pamoja ya kukuza biashara endelevu, huku tukiwa na mchango wa moja kwa moja katika uundaji wa ajira na kuboresha kipato kwa wafanyabiashara wadogo.

” Kwa kuingia makubaliano haya  GSM wanatupa nafasi ya kufanya biashara na  wadau wao wote. Yaani leo hii kama ni mdau  wa GSM ukihitaji kifaa chochote cha kusaidia katika biashara yako, taasisi ya EFTA itakupatia mkopo kuanzia wa  mwaka mmoja hadi miaka mitatu na hii itawezesha kumiliki magari au mitambo mabalimbali iytakayosaidia katika shughuli zao iwe   materkta kwa dhughuli za kilimo na Maroli kwa shughuli za usafirishaji “, amesema Asiel.

Amefafanua kuwa kwa mwaka jana pekee wameweza kutumia zaidi ya bilioni 48 kwa wakulima, wafanyabiashara na wajasiliamali  pia EFTA imeweza kuwakopesha mashine na mitambo wachimbaji wadogowadogo katika mikoa ya kanda ya ziwa alimaliza  Asiel.