
Mrembo anayetikisa mitandao ya kijamii kwa sasa, Queen Fraison, amefanya mahojiano ya kusisimua kupitia kipindi maarufu cha Bongo 255 kinachorushwa na Global TV.
Katika mahojiano hayo, Queen Fraison amegusia mambo mbalimbali kuhusu maisha yake ya sasa, mafanikio, changamoto, pamoja na tetesi zinazomuhusu.
Kauli zake zimezua gumzo mitandaoni huku baadhi wakimpongeza kwa ujasiri wake na wengine wakitaka kufahamu zaidi undani wa maisha yake.