×

Yanga Yahitaji Alama Moja Kutwaa Ubingwa, Simba Lazima Ishinde Dabi

Baada ya matokeo ya leo Jumapili Juni 22, 2025 sasa ni rasmi kuwa klabu ya Yanga inahitaji alama moja tu katika mchezo wao ujao dhidi ya Simba SC Uwanja wa Mkapa Juni 25, 205 ili kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara kwa msimu wa 2024/2025.

Kwa upande mwingine, Simba haina njia nyingine zaidi ya kushinda mchezo huo wa Kariakoo Derby ili kuendeleza matumaini ya kutwaa taji hilo. Huu ndio mchezo pekee uliosalia kwa kila timu, na unatarajiwa kuwa wa moto zaidi ya kawaida.

Matokeo ya mechi za leo.
Coastal 1️⃣–1️⃣ Tabora Utd
Fountain Gate 2️⃣–3️⃣ Azam FC
Mashujaa 0️⃣–0️⃣ JKT Tanzania
Namungo 5️⃣–0️⃣ Ken Gold FC
Pamba 1️⃣–1️⃣ KMC
Singida BS 3️⃣–3️⃣ TZ Prison
Yanga 5️⃣–0️⃣ Dodoma FC
Simba 1️⃣–0️⃣ Kagera Sugar