
Watu wanne wamefariki dunia na wengine wanne kujeruhiwa baada ya kugongwa na lori katika Kijiji cha Mtegu, Kata ya Sudi, Wilaya ya Lindi, mkoani Lindi.
Ajali hiyo imetokea majira ya saa moja usiku, baada ya lori lililobeba makaa ya mawe lenye namba za usajili T-157 EAV na tela lenye namba T-163 EAU, linalomilikiwa na Kampuni ya Specialized Hauliers Ltd, kuacha njia na kuwagonga watu waliokuwa wamekaa kwenye nyumba iliyokuwa pembezoni mwa Barabara Kuu ya Mingoyo–Mtwara.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Lindi, ACP John Imori, chanzo cha ajali hiyo bado hakijabainika na jeshi hilo linaendelea na uchunguzi.