
Kampuni ya kutengeneza magodoro ya TanFoam ambayo imejipatia umaarufu mkubwa kutokana na ubora wake inawakaribisha wananchi wote kwenye banda lao lililopo kwenye Maonesho ya 49 ya Kibiashara ya Kimataifa maarufu Sabasaba yanayoendelea kwenye Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere vilivyopo Barabara ya Kilwa jijini Dar.

Akizungumza kwenye maonesho hayo, Daniel Philipo Marko, Afisa Mauzo Kiwanda cha TanFoam amesema ukiwa ni msimu mwingine wa Sabasaba 2025, TanFoam kama kawaida yake huwa hawapoi wala hawaboi.

Daniel amesema anapenda kutumia nafasi hii kuwakaribisha wananchi mbalimbali kwenye banda lao lililopo kwenye Ukumbi wa Karume ili waweze kujipatia vocha ya punguzo la asilimia 10 kwa godoro walipendalo kuanzia tarehe 1 mpaka 31 mwezi huu.

“Njoo katika Viwanja vya Sabasaba tukuhudumie na kukupa bidhaa iliyo bora sana, TanFoam kama kawaida yetu tunasema alinunua Babu mpaka Mjukuu analitumia”. Alimaliza kusema Daniel.