×

Kocha Mpya Wa Yanga Afika Kimyakimya, Atarajiwa Kutambulishwa

Inaelezwa kuwa Kocha mpya wa Klabu ya Yanga ambaye anatarajiwa kuchukua mikoba ya Hamdi Miloud tayari ametua nchini kimyakimya na yupo katika hatua za mwisho za mazungumzo na viongozi wa juu wa klabu hiyo.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka chanzo cha kuaminika ndani ya Kamati ya Mashindano ya Yanga, kocha huyo tayari amesaini mkataba, na kilichobaki ni kutambulishwa rasmi mbele ya mashabiki na wanachama wa Yanga.

Kocha huyo anatajwa kuwa ni Julien Chevalier, raia wa Ufaransa, ambaye awali alikuwa akiinoa ASEC Mimosas ya Ivory Coast — klabu maarufu ambayo iliwahi kuwa chini ya wachezaji wanaofahamika vema ndani ya Yanga kama Stephane Aziz Ki, Yao Kouassi na Pacome Zouzoua.

Endapo atatambulishwa rasmi, Chevalier anatarajiwa kuja na falsafa mpya ya mchezo, huku akipewa jukumu la kuendeleza mafanikio ya klabu hiyo msimu mpya wa 2025/2026.