×

Donald Trump Kuhudhuria Fainali ya Kombe la Dunia la Vilabu FIFA

Rais wa zamani wa Marekani, Donald Trump, ametangaza kuwa atahudhuria fainali ya Kombe la Dunia la Vilabu la FIFA, itakayopigwa Jumapili kwenye Uwanja wa MetLife uliopo East Rutherford, New Jersey.

Trump alitoa kauli hiyo mwishoni mwa mkutano wa baraza la mawaziri Jumanne katika Ikulu ya White House, alipoulizwa kuhusu uwepo wake kwenye mchezo huo wa kihistoria.

“Nitaenda kwenye mchezo,” alisema Trump mbele ya waandishi wa habari.

Fainali hiyo itakutanisha klabu bingwa ya Ligi Kuu ya Uingereza, Chelsea, dhidi ya mshindi wa nusu fainali kati ya Paris Saint-Germain (Ufaransa) na Real Madrid (Uhispania), itakayochezwa Jumatano.

Michuano hiyo ya Kombe la Dunia la Vilabu, iliyochukua kipindi cha mwezi mzima, imekuwa gumzo ulimwenguni kutokana na ushindani mkali baina ya mabingwa wa mabara mbalimbali.