×

Simba Yampa Mkono wa Kheri Che Malone, Yampokea De Reuck Kutoka Sundowns

Klabu ya Simba imethibitisha kumpa mkono wa kwaheri beki wa kati Che Malone Fondoh almaarufu ‘Ukuta wa Yeriko’ kwa muda wote aliokuwa sehemu ya kikosi cha Wekundu hao wa Msimbazi.

Hatua hiyo inakuja masaa kadhaa baada ya Mnyama kushusha beki wa kati Rushine De Reuck, 29, raia wa Afrika Kusini akitokea Mamelodi Sundowns kwa mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza.

Ripoti zisizo rasmi zinaeleza kuwa Che Malone (26) raia wa Cameroon ambaye alijiunga na Mnyama mnamo 2023 akitokea Cotton Sport ya Cameroon amejiunga na klabu USM Alger ya Algeria kwa makubaliano ya pande zote mbili akitokea Simba Sc.