×

Bethidei ya Efm Sports Headquarters yabamba Dar

EFM (1) Watangazi wa kipindi cha Sports Head Quarter cha EFM Radio wakiendesha kipindi hicho wakati wa hafla ya maadhimisho ya mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake, hafla iliyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenye Ukumbi wa Sports Lounge, Posta jijini Dar. EFM (2) Mchezaji wa zamani wa Klabu ya Yanga, Ally Mayayi Tembele (kushoto) akihojiwa na mtangazaji wa kipindi hicho Ibrahim Masoud ‘Maestro’.
EFM (3) Mtangazaji  wa Kipindi cha Sports Head Quarter, Ibrahim Masoud (kushoto), akifanya mahojiano na mchezaji wa zamani wa Klabu ya Yanga, Sekilojo Chambua wakati wa maadhimisho hayo.
EFM (4) Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba SC. Said Tuli (kulia) akihojiwa.
EFM (5) Mmoja wa wadau wa kipindi hicho akihojiwa.
EFM (6) Rais wa BFT, Ostadh Yassin Abdallah akiohjiwa.
EFM (7) Bondia wa kike, Pendo Njau akizungumzia vitu vinavyomvutia kwenye kipindi cha Sports HQEFM (8) Mwandishi na mchambuzi wa habari za michezo, Edo Kumwembe (kulia) akihojiwa. 
EFM (9) Afisa Habari wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania ‘TFF’, Baraka Kizuguto (kushoto) naye akihojiwa.
EFM (10) Katibu wa Kmati ya Usajili ya Klabu ya Simba,  Mohamed Dewji akihojiwa.
EFM (11) Afisa habari wa Klabu ya Simba, Sande Haji Manara (wa pili kutoka kulia) akiteta jambo na waziri wa Habari, Vijana, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mh. Nape Nnauye.
EFM (12) Mkurugenzi wa EFM Radio, Francis Siza ‘Majay’ akimkaribisha Waziri Nape kwenye hafla hiyo.
EFM (13) Waziri Nape Nnauye akizungumza jambo.EFM (14)
EFM (15) Nape akikata keki.EFM (16)
EFM (17) Majay akimlisha keki Waziri Nape.
EFM (18)
EFM (19)
EFM (20) Nape akimlisha keki Maestro.
EFM (21) Majay akifungua zawadi ili amkabidhi waziri nape.
EFM (22) Majay akimkabidhi Nape zawadi ya kikombe.
EFM (23) Picha ya pamoja ya Waziri Nape na watangazaji wa EFM Radio.EFM (24) Nape akifungua shampeni
EFM (25)
EFM (26)
EFM (27)
EFM (28)
EFM (29)
EFM (30) Mziki ukafunguliwa.EFM (31) Burudani zikanogaEFM (32) Wakijiachia kwa raha zao.
EFM (33)Majay kwenye mashine.

 

KIPINDI cha EFM Sports Headquarters kinachosikika kupitia Radio ya Efm usiku wa kuamkia leo kiliadhimisha mwaka mmoja tangu kianze kurushwa ambapo pati yake ilifanyika katika Ukumbi wa Sports Lounge, Posta jijini Dar.

Kipindi hicho cha Sports HQ ambacho kinazungumzia michezo mbalimbali hapa nchini na nje kilianzishwa mwaka jana Februari 27, ambapo kinaongozwa na mkuu wa kitengo cha michezo redioni hapo Maulid Kitenge na msaidizi wake, Omari Katanga.

Pati hiyo ilihudhuriwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye, ambaye ndiye alikuwa mgeni rasmi katika bethidei hiyo ambayo ilianza majira ya saa 12 jioni na kumalizika usiku.

Akizungumza kwenye sherehe hiyo, Nape alisifia uwezo wa watangazaji wa kipindi hicho licha ya kuwa na muda mfupi kwa kuwa na uwezo wa kuhoji maswali ambayo yamekuwa na tija.

PICHA NA STORI: MUSA MATEJA/GPL

Leave a Comment