
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara anawatangazia Watanzania wenye sifa kuomba nafasi kumi na nne (14) za ajira baada ya kupata kibali kutoka Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora. Nafasi hizo ni kama ifuatavyo:
1.0 MWANDISHI MWENDESHA OFISI DARAJA LA II – NAFASI 2
Majukumu ya Kazi
i. Kuchapa barua, taarifa na nyaraka za kawaida na siri.
ii. Kupokea wageni na kuwasilisha shida zao pamoja na kuwaelekeza maeneo ya kusaidiwa.
iii. Kutunza kumbukumbu za matukio, miadi, tarehe za vikao na ratiba za kazi.
iv. Kutafuta majalada na nyaraka zinazohitajika.
v. Kupokea na kusambaza majalada kwa maofisa husika.
vi. Kukusanya, kutunza na kurejesha majalada.
vii. Kupanga dondoo na kuandaa maandalizi ya vikao.
viii. Kuandaa orodha ya mahitaji ya vifaa vya ofisi.
Sifa za Mwombaji
Kidato cha Nne (Form IV) au Kidato cha Sita (Form VI).
Stashahada (Diploma) ya Uhazili au Cheti cha NTA Level 6 – Uhazili.
Uwezo wa kuandika maneno 100 kwa dakika (Kiswahili na Kiingereza).
Ujuzi wa programu za kompyuta: Word, Excel, PowerPoint, Internet, Email na Publisher.
Ngazi ya Mishahara
TGS C
2.0 MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA II – NAFASI 5
Majukumu ya Kazi
i. Kuorodhesha barua zinazoingia kwenye daftari la kumbukumbu.
ii. Kuorodhesha barua zinazotoka nje ya Taasisi.
iii. Kusambaza majalada kwa watendaji.
iv. Kupokea majalada yanayorejeshwa masijala.
v. Kutafuta majalada/nyaraka zinazohitajika.
vi. Kurudisha majalada kwenye kabati/shubaka.
vii. Kufuatilia mzunguko wa majalada ndani na nje ya Taasisi.
Sifa za Mwombaji
Kidato cha Nne (IV) au Sita (VI).
Stashahada/Diploma (NTA Level 6) ya Utunzaji wa Kumbukumbu.
Ujuzi wa matumizi ya kompyuta.
Ngazi ya Mishahara
TGS C
3.0 DEREVA DARAJA LA II – NAFASI 7
Majukumu ya Kazi
i. Kukagua gari kabla na baada ya safari.
ii. Kuwapeleka watumishi kwenye safari za kikazi.
iii. Kufanya matengenezo madogomadogo ya gari.
iv. Kukusanya na kusambaza nyaraka.
v. Kujaza na kutunza taarifa za safari kwenye daftari la safari.
vi. Kufanya usafi wa gari.
vii. Kufanya kazi nyingine atakazoelekezwa.
Sifa za Mwombaji
Kidato cha Nne (Form IV).
Leseni ya Daraja E au C, iliyotumika kwa mwaka mmoja bila ajali.
Vyeti vya mafunzo ya uendeshaji (Basic Driving Course – VETA au chuo kinachotambuliwa).
Ngazi ya Mishahara
TGS B
MASHARTI YA JUMLA
i. Awe raia wa Tanzania, umri usiozidi miaka 45.
ii. Ambatanisha cheti cha kuzaliwa.
iii. Ambatanisha wasifu binafsi (CV) yenye anwani, namba za simu na majina ya wadhamini.
iv. Ambatanisha nakala za vyeti vya elimu na mafunzo kupitia Ajira Portal.
v. Hati za matokeo (Statement of Results, Provision Results) HAZIKUBALIKI.
vi. Waombaji wa udereva wawasilishe vyeti vya mafunzo ya udereva.
vii. Wasilisha picha mbili “passport size”.
viii. Waliosoma nje wahakikishe vyeti vimethibitishwa na TCU/NECTA/NACTE.
ix. Wastaafu wa Utumishi wa Umma hawaruhusiwi kuomba bila kibali cha Katibu Mkuu Kiongozi.
x. Waajiriwa wa kada za kuingilia hawaruhusiwi kuomba.
xi. Taarifa za kughushi zitachukuliwa hatua za kisheria.
xii. Mwisho wa kutuma maombi: 03 Disemba, 2025.
xiii. Barua ya maombi iandikwe kwa:
Mkurugenzi Mtendaji (W)
Halmashauri ya Wilaya Mtwara
S.L.P. 528
MTWARA
xiv. Maombi yote yawasilishwe kupitia:
👉 https://portal.ajira.go.tz/

