
Mabingwa wa Tanzania, Yanga wameanza kampeni zao za hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CAF Champions League) kwa kishindo baada ya kuibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya AS FAR Rabat ya Morocco, katika mchezo uliopigwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.
Mshambuliaji hatari wa Wananchi, Prince Dube, ndiye aliyeamua mchezo huo kwa kuiandikia timu yake bao pekee dakika ya 59, akiunganisha kwa ustadi pasi iliyowekwa katika eneo hatari na kuzamisha mpira kimiani bila kipa kuwa na ujanja.
Ushindi huo unaipa Yanga pointi tatu muhimu katika harakati za kusaka nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali, na pia unaendeleza rekodi nzuri ya timu hiyo inapocheza nyumbani kwenye michuano ya kimataifa.
Matokeo:
FT: Yanga SC 🇹🇿 1–0 🇲🇦 AS FAR Rabat
⚽ 59′ – Prince Dube
