The House of Favourite Newspapers
gunners X

Pacôme Zouzoua Apoteza Nafasi AFCON 2025 – Mashabiki Washangaa!

0

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast, Emerse Faé, ametangaza rasmi orodha ya wachezaji 25 watakaoiwakilisha nchi yao katika AFCON 2025 itakayofanyika Morocco.

Habari hiyo imekuwa pigo kwa mashabiki wengi waliokuwa na matumaini ya kumwona kiungo wa Yanga SC, Pacôme Zouzoua, akipata nafasi katika kikosi hicho. Taarifa rasmi zimebaini kwamba Zouzoua hatawezi kujiunga na timu, licha ya kiwango chake bora katika Ligi Kuu Tanzania Bara.

Wachambuzi walikuwa na matarajio makubwa kumwona Zouzoua akichangia kwenye safu ya kiungo ya Ivory Coast, kutokana na michango yake mikubwa na maendeleo ya kiwango cha juu alichonyesha msimu huu.

Ivory Coast, mabingwa wa AFCON 2023, wanasafiri Morocco wakiwa na lengo la kutetea taji lao, huku wakitajwa miongoni mwa timu zenye nafasi kubwa ya kufanya vizuri kwenye mashindano hayo.

Mashabiki wa Yanga na Tanzania kwa ujumla wanahuzunika kwa kutokuwapo kwa Zouzoua, lakini wengi wanasherehekea mafanikio yake Ligi Kuu na wanatarajia siku moja atakuwa sehemu ya kikosi cha AFCON.

APATA UVIMBE TUMBONI WAAMIA SEHEMU ya SIRI – YAGUNDULIKA KANSA – ATAKIWA KUCHANWA TUMBO AISHI…

Leave A Reply