The House of Favourite Newspapers

Dogo wa Miaka 5 Atengeneza Wimbo Albamu ya Kendrick Lamar

0

alicia-keys-600x800

Mtoto Egypt.

MTOTO wa nyoka naye ni nyoka! Unaweza kutumia msemo huu baada ya mtoto mastaa wa Marekani katika tasnia ya muziki, Alicia Keys na prodyuza Swizz Beatz anayeitwa Egypt (umri wa miaka mitano) ametengeneza ngoma iliyopo kwenye alabamu mpya ya Kendrick Lama ya untitled, unmastered.

Wazazi wake wamefarijika sana baada ya kupokea pongezi nyingi kutoka mashabiki wakionesha kuikubali kazi ya mtoto Egypt aliyomtengenezea wimbo mmoja kati ya nane ambazo Lamar anategemea kuziachia kwenye albamu yake hiyo mpya.kendrick-lamar-usher-jay-z-swizz-egypt-dean

Egypt ameonekana kufuata vyema nyao za baba yake Swizz za uprodyuza. Ametengeneza nusu ya pili ya wimbo wa “untitled 07”.

“Huu ni wakati mwafaka Baba!!!” alisema Swizz. “Hongera kwa mwanangu kwa kutengeneza wimbo wake mpya kwenye albamu ya Kendrick. Ana umri wa miaka mitano wowwwwwww @aliciakeys akimtazama mtoto wetu kipenzi. #blessingsonblessings thx #Kendrick kwa kuwekeza kwa ajili ya siku zijazo!!!”

Kwa sababu ilikuwa ni vigumu watu kuamini, wazazi wa Egypt waliamua kuweka vipande vya video mtandaoni zikionesha dogo huyo alivyokuwa akichezea vyombo studio wakati akiandaa wimbo huo.

Isikie ngoma yenyewe hapa. 

Leave A Reply