
Mwimbaji nguli wa muziki wa injili, Malikia Rose Muhando, amesema kuwa wakati anaachia wimbo wake maarufu “Facebook”, hakuwa na ufahamu wowote kuhusu mtandao huo wa kijamii.
Akizungumza katika mahojiano maalum na Global TV yaliyofanyika leo Januari 15, 2025, Rose ameeleza kuwa aliimba wimbo huo kwa kuongozwa na unabii, akielezea hali halisi ya maisha bila yeye mwenyewe kuelewa kikamilifu dhana ya Facebook kipindi hicho.