Na Mwandishi Wetu
PAMOJA na changamoto ya ukosefu wa ajira nchini, uchunguzi unaonesha kuwa idadi kubwa ya wahitimu hasa wa vyuo hawana sifa za kuajiriwa kutokana na vyuo vingi kuzalisha wasomi wenye vyeti visivyoambatana na uwezo na si wahitimu walioelimika kitaaluma.
Mkurugenzi wa Chuo cha Mlimani School of Professional Studies (MSPS) kinachofundisha taaluma mbalimbali, Hassan Ngoma anasema msingi wa tatizo la wasomi wengi kukosa kazi si ukosefu wa ajira bali wahitimu wengi kukosa sifa za kuajiriwa.
“Kampuni, idara, taasisi, wizara na viwanda hazihitaji wasomi wenye vyeti, zinahitaji watu wenye elimu, uwezo wa kufanya kazi. Vyuo vyetu vingi hapa nchini vinagawa vyeti, utakuta mwanafunzi amefaulu kwa alama A karibu masomo yote lakini hawezi kutafsiri kwa vitendo taaluma yake.
“Ufaulu wa A si kigezo cha kupata ajira, hakuna mwajiri anayetaka vyeti. Tuking’ang’ania kuamini kuwa tuna tatizo la ajira na kuacha kuangalia ubora wa vyuo vyetu katika kuwapa ujuzi wa kitaaluma wahitimu wake, tutalalamika mpaka mwisho wa dunia.
“Tumeshuhudia makampuni, idara, wizara na viwanda vingi vikitangaza nafasi za kazi, cha ajabu wanaopewa nafasi utashangaa kuambiwa ni wageni; kwa nini wageni? Wana sifa za kuajiriwa, mwajiri hachukui Ukenya au Utanzania wa mwajiriwa anachukua uwezo.
“Kwa kufahamu msingi huu wa changamoto, chuo chetu ambacho kimesajiliwa na NACTE, kimeamua kuacha kutoa elimu kwa mazoea, tumejipanga kuanzia sasa tuwe tunatoa wataalam ambao wataweza kuwa chaguo la kwanza la waajiri.
“Tumepanga mkakati kwa kila mwanafunzi wa ngazi ya stashahada (diploma) anayehitimu chuoni kwetu MSPS kwa kozi za Business Administration, Banking and Finance, Human Resources Management, Procurement and Supply, Accountancy, Information Technology na Journalism and Mass Communication, atoke na uwezo utakaomuwezesha kupata kazi kwa urahisi.
“Mpaka sasa chuo chetu kimejenga ushirikiano wa kutosha na wabia wa ajira wa taaluma zote tunazotoa ambao tutashirikiana nao moja kwa moja katika kuwasaidia wahitimu wetu kupata kazi na kukuza uzoefu wa kitaaluma.
“Tumebadilisha mfumo wote wa field, wanafunzi wetu tutawapangia sisi waende wapi na huko wakafanye nini kwa masilahi ya jamii. Mfano kama kijana kasomea masuala ya Accountancy tutampeleka kwenye vikundi vya Vicoba na Saccos mbalimbali ataonesha ujuzi wake huko kwa kipindi chote cha mafunzo akitoka huku atarejea chuoni na ripoti inayoonesha ufanisi aliouonesha huko.
“Mpango huu wa mageuzi ya utoaji elimu inayokidhi matakwa ya waajiri utaanza Machi 2016.
Naomba wazazi na wanafunzi wote ambao wameshindwa kuendelea na masomo ya kidato cha nne wafike chuoni kwetu kwa ajili ya usajili. Mawasiliano yetu ni kupitia namba 0715-200900.
“Kama nilivyosema chuo cha MSPS kimesajiliwa na NACTE kwa namba REG/BMG/036. Mazingira ya chuo ni mazuri, tuna vifaa vya kisasa vya kufundishia, hosteli bora, Wanafunzi wetu watafundishwa na walimu waliobobea na watapata fursa ya kupewa ujuzi wa ziada kutoka kwa wajasiriamali wazoefu, waandishi wa habari nguli na wawekezaji wa ndani na nje ya nchi,” alisema Ngoma.
HADITHI ZA KUSISIMUA NA MBINU ZA UJASIRIAMALI, INGIA NA LIKE PAGE YA FACEBOOK YA ERIC SHIGONGO===>https://www.facebook.com/shigongotz/
KWA HABARI ZA KITAIFA, KIMATAIFA, MASTAA NA MIKASA YA KUSISIMUA TUFOLLOW
INSTAGRAM===>https://www.instagram.com/globalpublishers/
TWITTER===>https://twitter.com/GlobalHabari
FACEBOOK===>https://www.facebook.com/GlobalPublishers
YOU TUBE===>https://www.youtube.com/user/uwazi1