The House of Social Media
gunners X

Rais wa Iran Azishutumu Marekani, Israel na Ulaya Kuhusiana na Machafuko

0
Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian

TEHRAN, Iran – Rais wa Iran, Masoud Pezeshkian, amezishutumu vikali Marekani, Israel, na baadhi ya mataifa ya Ulaya kwa kutumia matatizo ya kiuchumi ya nchi hiyo kuendeleza machafuko yaliyolenga “kusambaratisha taifa.”

Akizungumza kwenye televisheni ya serikali siku ya Jumamosi, Januari 31, 2026, Pezeshkian alidai kuwa malalamiko ya raia kuhusu mfumuko wa bei na kupanda kwa gharama za maisha yalitumika na mataifa ya Magharibi kama kigezo cha kuingilia kati na kueneza chuki miongoni mwa Wairani.

“Trump, Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu na Wazungu walijiingiza kwenye matatizo yetu, wakachochea, na walikuwa wakitafuta – na bado wanatafuta – kuigawanya jamii… Waliwaleta mitaani na walitaka, kama walivyosema, kusambaratisha nchi hii, kuitumbukiza kwenye mizozo na chuki miongoni mwa watu na kusababisha mgawanyiko,” alisema Pezeshkian.

Rais wa Marekani, Donald Trump, ameendelea kutoa kauli za kuunga mkono waandamanaji huku akitishia kuchukua hatua za kijeshi iwapo mauaji na ghasia yataendelea. Hata hivyo, Washington inaendelea kushikilia msimamo wake kuwa mazungumzo yoyote yanapaswa kuzingatia Iran kuachana na mpango wake wa silaha za nyuklia.

Kuhusiana na hili, Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Abbas Araqchi, amesisitiza kuwa suala la silaha halitakuwa mada yoyote katika mazungumzo.

Juhudi za kidiplomasia zinazohusisha mataifa ya kanda, ikiwemo Uturuki, Saudi Arabia, na Falme za Kiarabu, zinaendelea ili kuepusha mzozo huu kugeuka kuwa vita kamili kati ya Washington na Tehran.

Leave A Reply