
Dar es Salaam – Benki ya Stanbic Tanzania imetambulisha rasmi huduma ya Lipa Simpo kwa wateja, ikiruhusu kufanya malipo moja kwa moja kupitia Stanbic App au USSD *150*29#.

Hii inakuja baada ya mfumo wa Lipa Simpo kuwepo kwa muda, ukiruhusu wajasiriamali na biashara kupokea malipo kupitia QR kutoka benki na mitandao yote nchini.

Kupitia huduma hii ya ufanyaji malipo, wateja wanaweza kulipa bidhaa na huduma kwa sekunde chache, salama na moja kwa moja kutokea kwenye akaunti zao za Benki ya Stanbic, bila kuhitaji pesa taslimu au kubeba chenji.
Akizungumza akiwa Mwenge Dar es Salaam leo, katika ziara maalum ya kutembelea wateja na kutoa elimu juu ya huduma hii, Mkuu wa Huduma za Kidijitali, Stanbic Bank, Edward Balandya amesema kuwa:
“Kwa kipindi maalum hadi Aprili 2026, miamala ya zaidi ya TZS 40,000 itatozwa ada ya TZS 1,000 tu, ikiruhusu wateja kulipa kiasi kikubwa kwa gharama ndogo.”
“Tunawashauri wateja kupakua Stanbic App ili kuanza kutumia Lipa Simpo na kufurahia malipo haraka, salama na rahisi.”