Benki ya NMB yatoa milioni 25 kwa Timu ya Taifa Mpira wa Magongo
Global Publishers
March 8, 2016
0 Comments
Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas akimkabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Milioni 25 Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati) ikiwa ni fedha ya udhamini wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Magongo chini ya miaka 21 inayoelekea Namibia kushiriki mashindano ya kufuzu KOmbe la Afrika mpira wa magongo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa mpira wa Magongo, Abraham Sykes akipokea kwa niaba ya timu hiyo. NMB mbali ya udhamini huo imetoa mabegi maalumu kwa kila mchezaji wa timu hiyo kwa ajili ya safari hiyo.
- Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akikabidhi bendera kwa Nahodha wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Magongo chini ya miaka 21, Elieza Jeremiah (wa pili kushoto). Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa mpira wa Magongo, Abraham Sykes akishuhudia tukio hilo. Timu ya Taifa ya Mpira wa Magongo chini ya miaka 21 inaondoka nchini Machi 3, 2016 kuelekea nchini Namibia kushiriki mashindano ya kufuzu Kombe la Afrika mpira wa magongo chini ya udhamini wa NMB.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akizungumza kabla ya kupokea mfano wa hundi ya Shilingi Milioni 25 iliyotolewa na NMB ikiwa ni fedha ya udhamini wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Magongo chini ya miaka 21 inayoshiriki mashindano ya kufuzu Kombe la Afrika mpira wa magongo yatakayofanyika nchini Namibia. Kulia ni Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas.
Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas (kulia) akizungumza kabla ya kukabidhi mfano wa hundi ya Shilingi Milioni 25 ikiwa ni fedha ya udhamini wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Magongo chini ya miaka 21 inayoelekea Namibia kushiriki mashindano ya kufuzu Kombe la Afrika mpira wa magongo. Kushoto ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye.
-
Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Mpira wa Magongo chini ya miaka 21 nchini Tanzania wakipiga picha na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye pamoja na viongozi wao mara baada ya kukabidhiwa bendera ya taifa leo jijini Dar es Salaam.

- Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Mchezo wa mpira wa Magongo, Abraham Sykes, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye na Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya NMB, Waziri Barnabas wakijibu maswali ya wanahabari katika hafla ya timu hiyo kukabidhiwa bendera na udhamini wa NMB.