Kampuni ya kimataifa ya michezo ya kubashiri ifahamikayo kama Golden Matrix Group, imebadilisha rasmi jina lake na kuwa Meridian Holdings Inc. Kuanzia sasa, kampuni hiyo inaanza kufanya biashara katika soko la Nasdaq Capital Market kwa alama mpya ya hisa MRDN. Hatua hii inaashiria mwanzo wa enzi mpya ya kimkakati na kifedha kwa kampuni hiyo katika jukwaa la kimataifa.
Mabadiliko ya jina yanaendana na utambulisho wa chapa yake ya Meridianbet, ambayo imeendelea kupanua wigo wake katika masoko mbalimbali duniani. Kupitia muundo wake wa sasa, Meridian Holdings Inc. inasimamia taasisi sita muhimu za Meridianbet, Expanse Studios, RKings, Classics for a Cause, GMAG na Mexplay.
Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi! Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.
Mageuzi haya yanakuja kufuatia mafanikio ya hivi karibuni ya Meridianbet kukamilisha ununuzi wa asilimia 100 wa Fairbet Ltd. nchini Malta. Kupitia hatua hiyo, kampuni imeongeza mara mbili uwepo wake katika maeneo ya Malta na Gozo, jambo lililoimarisha nafasi yake kama mdau mkubwa katika soko hilo la Ulaya.
Sambamba na mabadiliko ya utambulisho, Meridian Holdings Inc. inapanga kutekeleza mpango wa kuunganisha hisa ili kuboresha muundo wa hisa zake na kuongeza mvuto kwa wawekezaji wa taasisi. Lengo la mkakati huu ni kuimarisha thamani ya hisa sokoni na kuendana na viwango vya kimataifa vya sekta ya michezo ya kubahatisha.
Afisa Mtendaji Mkuu, Zoran Milosevic, alieleza kuwa uamuzi wa kubadilisha jina unalenga kuimarisha uwiano kati ya chapa na muundo wa kampuni kwa manufaa ya wanahisa na wadau wote. Alisisitiza kuwa mafanikio ya upanuzi nchini Malta ni ushahidi wa mkakati madhubuti wa ukuaji wa kimataifa. Kwa mabadiliko haya, Meridian Holdings Inc. inaweka msingi imara wa ushindani na mafanikio katika soko la dunia.