×

Video: Rais Samia Amzawadia Gari Mama Kanumba

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amemzawadia gari aina ya Toyota Harrier mama wa marehemu Steven Kanumba, kama ishara ya kutambua mchango mkubwa wa mwanaye katika kukuza tasnia ya filamu nchini.

Gari hilo limekabidhiwa kwa niaba ya Rais na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, katika viwanja vya Barafu Mbulahati Grounds wakati wa maadhimisho ya International Women’s Day yaliyofanyika hapo.

Zawadi hiyo imelenga kuenzi na kuthamini mchango mkubwa alioutoa marehemu Steven Kanumba katika kukuza na kuutangaza ulimwengu wa filamu za Kitanzania, maarufu kama Bongo Movie.

Leave a Comment