
Rais mstaafu wa Botswana, Ian Khama (73), bado anaonesha kiwango kikubwa cha uimara wa mwili kwa kuendelea kufanya mazoezi makali ya kijeshi kila wiki.
Mazoezi hayo ambayo mara nyingi hufanywa na wanajeshi au makomandoo, yanaonekana kuwa sehemu ya maisha yake ya kila siku licha ya umri wake na kumaliza kipindi chake cha uongozi.

Wengi wamekuwa wakishangazwa na uwezo wake wa kufanya mazoezi hayo ambayo hata baadhi ya watu wenye umri mdogo hushindwa kuyafanya.
Nidhamu ya kijeshi ambayo Khama aliijenga tangu akiwa jeshini inaonekana kuendelea kumsaidia kudumisha afya, nguvu na uthabiti hata baada ya kuondoka madarakani.