×

Polisi Wafanya Uchunguzi Baada ya Nyumba ya Rihanna Kushambuliwa

Polisi wa Los Angeles nchini Marekani wanafanya uchunguzi baada ya nyumba ya Rihanna iliyopo Beverly Hills kushambuliwa kwa risasi Jumapili mchana.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Marekani, tukio hilo lilitokea majira ya saa 7 mchana kwa saa za huko, ambapo mshukiwa alifyatua takribani risasi 10 kutoka ndani ya gari lililokuwa upande wa pili wa barabara karibu na jumba hilo.

Maafisa wa polisi wanasema risasi moja ilipenya ukuta wa nyumba hiyo, ambayo Rihanna anaishi pamoja na mwenzi wake, rapa A$AP Rocky, pamoja na watoto wao.

Polisi wamethibitisha kuwa Rihanna alikuwa ndani ya nyumba wakati wa tukio hilo, lakini hakupata majeraha.

Hadi sasa, mwimbaji huyo bado hajatoa tamko rasmi kuhusu tukio hilo.

🔴 Tufuatilie kupitia YouTube ya Global TV, like, comment ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.

CHINA INASUBIRI SIMU ya IRAN ya KUTAKA MSAADA IKAMSAIDIE – IRAN INAJIAMINI INAWEZA KUJILINDA YENYEWE

Leave a Comment