
Shirikisho la Soka la Senegal (FSF) limekosoa uamuzi wa CAF kuwatangaza kupoteza mechi ya fainali ya AFCON 2025 , na hivyo ushindi wa mezani wa mabao 3–0 kutolewa kwa Morocco .
FSF limeahidi kupeleka rufaa kwa Mahakama ya Michezo (CAS) huko Lausanne. Katibu Mkuu wa FSF, Abdoulaye Sow, amesema:“Kombe halitaondoka nchini Senegal ina haki, na ushindi upo upande watu.”

Wachezaji pia walionyesha hisia za hasira na uchungu:
-
Idrissa Gana Gueye alisisitiza kuwa vyeo na vikombe vinaisha, lakini heshima ya mashabiki na jamii ndiyo muhimu zaidi.
-
El Hadji Malick Diouf, ambaye alihusika kwa kosa la penati, aliongeza:
“Kombe linashindaniwa uwanjani, sio kwa barua pepe.”
-
Habib Diarra aliweka picha akiwa na kombe kwenye Instagram, kuonyesha kwamba timu haiwezi kukata tamaa.
Bodi ya Rufaa ya CAF ilitangaza kwamba Senegal imepoteza fainali, na matokeo kuandikwa kama 3-0 kwa Morocco. Shirikisho la Soka la Morocco limekubali uamuzi, lakini limeeleza kwamba rufaa yao ilikuwa juu ya kutekeleza kanuni za mashindano pekee, si kupinga utendaji wa timu yoyote.