
Habari njema kwa mashabiki wa ubashiri. Expanse Studios wamechukua hatua kubwa tena sokoni kwa kutangaza ushirikiano wao mpya na Stake, moja ya majukwaa makubwa duniani ya michezo ya kubahatisha. Baada ya kujijengea heshima kubwa kupitia kazi zao na kampuni mbalimbali kama Meridianbet, sasa wanawaletea wachezaji uzoefu mpya uliojaa ubunifu na nafasi nyingi za kushinda kupitia jukwaa la Stake.
Kwa muda mrefu, Expanse Studios wamekuwa wakitamba kwa kutengeneza michezo inayovutia na yenye ushindani mkubwa. Michezo yao imekuwa gumzo miongoni mwa wabashiri kutokana na ubora wake na namna inavyotoa burudani ya kipekee na sasa, wachezaji wa Stake wanapata nafasi ya kufurahia michezo kama Gates of Olympia, Super Heli, PIA Premium, Keno, Zombie Apocalypse na Wild white whale moja kwa moja, bila vikwazo.
Mafanikio ya Expanse yanatokana na msingi imara wa kampuni mama inayowaongoza, Meridian Holdings Inc., ambayo pia inasimamia majukwaa mengine makubwa ya ubashiri duniani kama Meridianbet, Rkings na Mexplay. Hii inaonyesha wazi kuwa wanachokileta sokoni sio tu mchezo, bali ni uzoefu ulioboreshwa na kuthibitishwa kimataifa.
Akizungumzia ushirikiano huo, mtendaji mkuu wa Expanse Studios Damjan Stamenkovic alieleza kuwa hii ni hatua ya kimkakati ya kupanua huduma zao na kuwafikia wachezaji wengi zaidi duniani. Kupitia teknolojia ya kisasa na mifumo ya usambazaji, wanahakikisha kuwa kila mchezaji anapata burudani ya kiwango cha juu na nafasi halisi za ushindi.
Kwa zaidi ya washirika 1,300 duniani na zaidi ya michezo 70 ya kipekee, Expanse Studios wanaendelea kuthibitisha kuwa wao ni kinara wa mabadiliko katika sekta ya ubashiri. Ushirikiano huu na Stake ni ishara tosha kuwa mambo makubwa yanakuja na sasa ni wakati wako kujiunga, kucheza kwa akili na kushinda zaidi.