
Serikali ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Ofisi ya Rais, Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma imetangaza jumla ya nafasi 630 za ajira kwa Watanzania wenye sifa na uwezo wa kujaza nafasi mbalimbali katika taasisi za serikali (MDAs na LGAs) pamoja na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Kwa mujibu wa tangazo lenye Kumb. Na. JA.9/259/01/C/24 la tarehe 22 Aprili 2026, nafasi hizo zinahusisha kada mbalimbali. Miongoni mwa nafasi zilizotangazwa ni Walimu wa Elimu Maalum (7), Waandishi Waendesha Ofisi Daraja la II (243), Daktari wa Mifugo Daraja la II (1), Wakadiriaji Ujenzi Daraja la II (55) pamoja na Madereva Daraja la II (296).
Aidha, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia nayo imetangaza nafasi za wakufunzi wasaidizi katika fani tofauti, zikiwemo Uandaaji wa Chakula (nafasi 5), Ushonaji na Ubunifu wa Mitindo (nafasi 10) pamoja na Uchomeleaji na Utengenezaji wa Vyuma (nafasi 13).
Serikali imeweka masharti ya jumla kwa waombaji, ikiwa ni pamoja na umri usiozidi miaka 45. Pia imewahimiza watu wenye ulemavu kujitokeza kuomba nafasi hizo huku wakitakiwa kubainisha hali zao katika mfumo wa maombi.
Mwisho wa kutuma maombi ni leo Aprili 4, 2026.
Fungua link hii kusoma zaidi >>>