×

Kongamano la Kiswahili Duniani Lafunguliwa Rasmi Jijini Arusha

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, akiwa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) leo Machi 24, 2026.

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Hemed Suleiman Abdulla, ameungana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, katika uzinduzi wa Kongamano la Tano la Idhaa za Kiswahili Duniani linalofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC) leo Machi 24, 2026.

Kongamano hilo muhimu limeandaliwa na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), likilenga kuwakutanisha wadau wa Idhaa za Kiswahili kutoka ndani na nje ya nchi ili kujadili maendeleo, changamoto na fursa za kukuza lugha ya Kiswahili kupitia vyombo vya habari.

Tukio hilo linafanyika kuanzia Machi 24 hadi 27, 2026 katika ukumbi wa AICC, Jijini Arusha, likitarajiwa kuwa jukwaa muhimu la kubadilishana uzoefu na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika kuendeleza Kiswahili duniani.

Kongamano hilo la 5 la Idhaa za Kiswahili Duniani limeandaliwa na Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA), likiwakutanisha wadau wa Idhaa za Kiswahili kutoka ndani na nje ya nchi linalofanyika kuanzia tarehe 24 hadi 27 Machi, 2026 katika Ukumbi wa Kituo cha Kimataifa cha Mikutano (AICC), Jijini Arusha.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, akiongea watika uzinduzi wa Kongamano la Tano la Idhaa za Kiswahili.

Leave a Comment