
Aliyekuwa Mkuu wa Majeshi ya Marekani (Army Chief of Staff), Randy George, ameaga rasmi kwa ujumbe mzito akisisitiza kuwa wanajeshi wanahitaji viongozi jasiri wenye maadili, kufuatia kuondolewa kwake madarakani.
Katika barua pepe yake ya mwisho kwa maafisa wa Pentagon, George alisema ni heshima kubwa kuongoza wanajeshi na akaeleza kuwa ana imani wataendelea kufanya kazi kwa bidii, ubunifu na kuondoa urasimu ili kuwapa wanajeshi kile wanachohitaji kushinda vitani.
Hatua ya kuondolewa kwake ilikuja baada ya Waziri wa Ulinzi, Pete Hegseth, kumtaka ajiuzulu na kustaafu mara moja. Inaelezwa kuwa Hegseth anataka kiongozi mpya atakayetekeleza maono yake pamoja na ya Rais Donald Trump kuhusu mwelekeo wa jeshi.
Katika ujumbe wake, George alisisitiza:
- Wanajeshi wa Marekani ni bora duniani
- Wanastahili mafunzo magumu
- Wanahitaji viongozi wenye ujasiri, maadili na uthabiti
Kwa sasa, nafasi yake inashikiliwa kwa muda na Christopher LaNeve, ambaye ni Naibu Mkuu wa Majeshi.
George, ambaye aliteuliwa kushika wadhifa huo mwaka 2023 (nafasi ambayo kawaida hudumu miaka minne), anaondoka kabla ya muda wake kuisha, hatua inayoonyesha mabadiliko makubwa ndani ya uongozi wa jeshi la Marekani chini ya utawala wa sasa.