×

Video: Marekani Yaokoa Askari Wake Ndani ya Iran Baada ya Ndege Kupigwa

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuwa mwanajeshi wa Marekani aliyekuwa amepotea baada ya ndege ya kivita aina ya F-15E Strike Eagle kupigwa nchini Iran, ameokolewa salama katika operesheni maalum ya kijeshi.

Kwa mujibu wa maafisa wa Marekani, operesheni hiyo ya uokoaji ilifanyika mapema Jumapili na kuhusisha vikosi maalum, ndege za kivita pamoja na helikopta kadhaa, ikiwa ni moja ya oparesheni hatari na kubwa kuwahi kufanywa na jeshi la Marekani.

Kupitia ujumbe wake kwenye mtandao wa kijamii, Trump alisema: “Tumempata! Yupo salama licha ya kuwa na majeraha madogo.”

Awali, ndege hiyo ya kivita ilidunguliwa na vikosi vya Islamic Revolutionary Guard Corps siku ya Ijumaa, ikiwa na wahudumu wawili. Rubani aliweza kujiokoa mapema na kuokolewa, huku afisa wa pili akiwa amepotea kwa muda kabla ya kupatikana.

Inaelezwa kuwa wakati wa operesheni hiyo, vikosi vya Marekani vilitumia mashambulizi ya anga kuzuia wanajeshi wa Iran wasikaribie eneo alikokuwa amejificha askari huyo, ambaye alikuwa na silaha ndogo pekee ya kujilinda.

Baada ya kuokolewa, askari huyo alipelekwa nchini Kuwait kwa ajili ya matibabu.

Leave a Comment