
Tume ya Rais ya kuchunguza matukio ya kabla na baada ya uchaguzi wa Oktoba 29, 2025 imeomba kuongezewa tena muda wa siku nyingine 21 kukamilisha kazi.
Nyongeza hiyo ya muda, ni ya pili kwa tume hiyo ambayo Februari 20, 2026, iliongezewa siku 42 kukamilisha kazi yake, baada ya siku 90 za awali kuisha.
Baada ya kuongezewa muda kwa mara ya pili, tume hiyo inatarajiwa kukamilisha kazi hiyo kabla ifikapo April 24, 2026.
