
Kampuni ya Qualcomm Incorporated imetangaza rasmi kampuni changa 10 zilizochaguliwa kushiriki katika toleo la nne la Mpango wa Ushauri wa Qualcomm® Make in Africa.
Kupitia mpango huu, Qualcomm inaendelea kuthibitisha dhamira yake ya kuimarisha mfumo wa teknolojia ya hali ya juu barani Afrika kwa kutoa ushauri, mafunzo, na mipango ya kukuza miliki bunifu (IP). Mpango huu ni sehemu ya Qualcomm Africa Innovation Platform, unaolenga kusaidia maendeleo ya ubunifu unaotumia teknolojia za kisasa.
Washiriki wa mwaka huu watawezeshwa katika maeneo ya teknolojia kama vile Edge AI/ML, uchakataji wa kompyuta (compute), IoT (Mtandao wa Vitu), pamoja na jukwaa la maendeleo ya AI la Qualcomm kupitia Arduino.
Katika fainali ya mpango huo, kampuni moja itapata ruzuku kutoka mfuko wa Qualcomm for Good, huku kampuni zote zitakazokamilisha mpango zikitarajiwa kupata posho ya dola za Marekani 5,000.
Mbali na hilo, Qualcomm itatoa rasilimali mbalimbali ikiwemo mwongozo wa kubuni bidhaa kwenye majukwaa ya Arduino AI, ushauri wa biashara, upatikanaji wa wataalamu wa uhandisi, pamoja na elimu ya bure ya miliki bunifu kupitia L2Pro Africa.
Kwa mwaka 2026, kampuni changa 10 zimechaguliwa kutoka zaidi ya maombi 1,200 yaliyowasilishwa kutoka nchi zaidi ya 45 za Afrika. Uchaguzi huo ulizingatia uwezo wa kutumia teknolojia za kisasa katika kutatua changamoto halisi kupitia suluhisho bunifu. Sekta zilizowakilishwa ni pamoja na kilimo, teknolojia saidizi, miji janja, miundombinu janja, usafiri wa magari ya umeme (EV), na elimu.
Kampuni Changa Zilizochaguliwa 2026:
- Amperra Charging Company (Namibia) – Mfumo wa kuchaji magari ya umeme unaotumia AI
- Anatsor Ltd (Nigeria) – Mfumo wa kidijitali wa usimamizi wa ufugaji wa kuku
- D Olivette Labs (Nigeria) – Jukwaa la bio-intelligence kwa kilimo endelevu
- Mindora Corporation (Zimbabwe) – Kibodi ya Braille kwa watu wenye uoni hafifu
- MVUTU (Jamhuri ya Kongo) – Mfumo wa kuhifadhi mazao kwa baridi unaotumia nishati ya jua na IoT
- QualiKeeper Investments Ltd (Zambia) – Mfumo wa AIoT wa kufuatilia mifugo vijijini
- SafeSip (Tanzania) – Suluhisho la maji salama kwa kutumia teknolojia janja
- Sesi Technologies Ltd (Ghana) – Kifaa cha AI kutathmini ubora wa kakao
- TWave Ltd (Uganda) – Mfumo wa kulisha samaki unaotumia nishati ya jua
- Zerobionic (Kenya) – Roboti saidizi kwa watu wenye ulemavu
Akizungumzia mpango huo, Wassim Chourbaji alisema ubunifu wa kampuni changa za mwaka huu unaonyesha ukuaji mkubwa wa mfumo wa ubunifu barani Afrika, akisisitiza mchango wa teknolojia kama Edge AI na 5G katika kutatua changamoto za bara hili.
Kwa upande wake, Fabio Violante alisema majukwaa ya Arduino kama Arduino® UNO™ Q yanawezesha wabunifu kubadilisha mawazo yao kuwa suluhisho janja kwa haraka.
Washiriki pia watapata msaada wa maendeleo ya bidhaa, ushauri wa kulinda miliki bunifu, pamoja na msaada wa usajili wa hataza kupitia Adams & Adams.
Mpango huo unashirikiana kwa karibu na African Telecommunications Union, ambapo Katibu Mkuu John Omo alieleza kuwa mpango huo unawezesha wabunifu wa Afrika kutumia teknolojia kutatua changamoto za ndani kwa ufanisi.
Kwa maelezo zaidi gusa hapa
