
Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) imetoa wito kwa Serikali, sekta binafsi na jamii kushirikiana kikamilifu kukabiliana na tatizo la pombe haramu nchini.
TBL imesema pombe haramu inaendelea kuhatarisha afya za wananchi kutokana na kutengenezwa bila viwango, hali inayoweza kusababisha madhara makubwa ikiwemo vifo. Aidha, imeeleza kuwa biashara hiyo inaikosesha Serikali mapato ya zaidi ya shilingi trilioni 1 kila mwaka na kuvuruga ushindani wa haki sokoni.
Mkurugenzi Mtendaji wa TBL, Michelle Kilpin, amesema suluhisho la changamoto hiyo linahitaji utekelezaji madhubuti wa sheria, sera thabiti za kodi pamoja na elimu kwa umma.
Amesisitiza kuwa mapambano dhidi ya pombe haramu ni jukumu la pamoja, huku TBL ikiendelea kuzalisha bidhaa salama na kuhamasisha matumizi ya kuwajibika.