
Mbunge wa Buchosa, Eric Shigongo, amefanya tathmini ya bajeti ya Wizara ya Vijana iliyowasilishwa leo Bungeni na Waziri Joel Nanauka.
Akizungumza baada ya uwasilishaji huo, Shigongo amesisitiza kuwa bado kuna sababu kubwa ya kuongeza nguvu katika kushughulikia changamoto zinazowakabili vijana nchini, huku akitaka sauti ya vijana isikilizwe na kupewa kipaumbele katika mipango ya maendeleo ya taifa.
Ameeleza kuwa vijana ndio nguvu kazi kubwa ya taifa, hivyo bajeti hiyo inapaswa kuzingatia mahitaji yao halisi ikiwemo ajira, ujuzi na fursa za kiuchumi.
Shigongo ametoa wito kwa serikali kuhakikisha kuwa sera na mipango ya vijana inatekelezwa kwa ufanisi ili kuleta mabadiliko chanya na endelevu kwa kizazi cha sasa na kijacho.
🔴 Usisahau ku-like, comment na kutufollow ili kuendelea kuhabarika kila siku kwa habari mbalimbali zenye ukweli na uhakika.
View this post on Instagram