×

SUA Yatangaza Nafasi Mpya za Ajira kwa Wahadhiri na Watafiti, Mwisho wa Maombi Mei 5, 2026

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimetangaza nafasi mbalimbali za kazi za kitaaluma kwa Watanzania wenye sifa stahiki, katika fani tofauti za kilimo, elimu, biashara na sayansi ya mazingira.

SUA, kilichoanzishwa mwaka 1984 kwa Sheria ya Bunge Na. 6 na kupewa Hati ya Chuo Kikuu mwaka 2007, kinasema dhamira yake ni kuwa chuo kinachoongoza katika kutoa elimu bora, ujuzi na ubunifu katika sekta ya kilimo na sayansi zinazohusiana.

Nafasi zilizotangazwa

Nafasi hizo ni pamoja na:

  • Assistant Lecturer katika:
    • Animal Science
    • Agricultural Extension
    • Wildlife Management
    • Community Development
    • Curriculum and Instruction
    • Tourism Management
    • Linguistics
  • Research Fellow Trainee katika:
    • Aquaculture
    • Agricultural Extension
    • Forest Engineering
  • Tutorial Assistant katika:
    • Community Development
    • Literature
    • Banking
    • Trade

Sifa za Waombaji

Waombaji wanatakiwa kuwa na:

  • Shahada za Uzamili (Master’s Degree) au Shahada ya Kwanza kulingana na nafasi husika
  • GPA ya angalau 4.0 kwa Master’s na 3.8 kwa Bachelor’s
  • Uwezo wa kufundisha, kufanya utafiti na kushiriki shughuli za kijamii na kitaaluma

Masharti Muhimu

  • Waombaji wawe raia wa Tanzania wasiozidi umri wa miaka 45
  • NIDA number ni lazima
  • Maombi yafanywe kupitia Ajira Portal pekee
  • Waombaji watakaobainika kutumia vyeti feki watachukuliwa hatua za kisheria
  • Mwisho wa kutuma maombi ni Mei 5, 2026

Soma zaidi >>> NAFASI ZA KAZI CHUO KIKUU CHA KILIMO CHA SOKOINE(SUA) 23-04-2026

Leave a Comment