
Mtanzania Neema Anderson aliyetoroka kupitia dirishani kwenye ghorofa ya pili nchini Oman amerejea nchini Tanzania na kuzungumza mengi na Global TV.
Neema ameeleza kuwa alienda nchini Oman kwa ajili ya kufanya kazi za ndani ili apate fedha za kumsaidia mama yake mzazi na kujikwaumua kwenye umaskini, lakini isivyo bahati hakupata alichokitaka.
Neema anaeleza kuwa alipokuwa kwa bosi wake alipitia changamoto nyingi ikiwemo kunyimwa chakula na kutolipwa baadhi ya pesa zake za mshahara, jambo lililomfanya aamue kutoroka ili arejee nchini Tanzania.