×

Dabi ya Kariakoo: Simba na Yanga Kuamua Hatima ya Ubingwa Leo!

Leo, Mei 03, 2026, dimba la Meja Janerali Isamuhyo jijini Dar es Salaam litashuhudia pambano la kihistoria kati ya Simba  na Yanga katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Huu ni mchezo wa duru ya pili wa ligi ambapo timu zote mbili zitakuwa zikisaka ushindi muhimu katika mbio za ubingwa.

Simba wanahitaji ushindi ili kupunguza pengo la pointi 5 dhidi ya Yanga, ambao wako kileleni na wanahitaji matokeo ya ushindi ili kuendeleza matumaini ya kutetea taji lao la ligi.

Mchezo huu ni muhimu kwa timu zote mbili, kwani mshindi ataongeza nafasi nzuri ya kushinda ubingwa wa msimu huu.

Huu utakuwa ni mkutano wa nne wa msimu kati ya timu hizi, ambapo Yanga walishinda 1-0 kwenye Nguo ya Jamii na kutafuta sare tasa kwenye mchezo wa duru ya kwanza wa ligi kuu.

Simba , kwa upande mwingine, walijibu kwa ushindi wa 1-0 kwenye fainali ya Kombe la Muungano, na hivyo kutwaa taji hilo la kombe.

Simba  wana wasiwasi kuhusu baadhi ya wachezaji wake, winga Anicet Oura, viungo Yusuph Kagoma, Alassane Kante, pamoja na mabeki Ismael Touré na Nickson Kibabage, ambao walitoka kwa maumivu kwenye fainali ya Kombe la Muungano. Hata hivyo, taarifa kutoka kwa viongozi wa timu hiyo zinasema kwamba wachezaji hao watakuwa tayari kwa Dabi hii.

Kwa upande wa Yanga timu hiyo itakosa huduma ya kiungo Mudathir Yahya, ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi tatu, pamoja na Mohammed Hussein ‘Zimbwe Jr’ ambaye atakosekana kutokana na majeraha.

Uwanja wa Meja Janerali Isamuhyo unatarajiwa kuwa sehemu ya kihistoria kwa sababu Dabi ya Kariakoo itachezwa hapo kwa mara ya kwanza. Hii ni nafasi ya kipekee kwa mashabiki wa soka kuishuhudia mechi hii muhimu katika uwanja huu mpya.

Mchezo:

  • Simba SC 🆚 Yanga SC
  • Wakati: 18:00
  • Mahali: Meja Janerali Isamuhyo, Dar es Salaam

MSIMAMO NBC 🔝2️⃣

  1. YANGA SC — Mechi 19 — Pointi 47 (+43)
  2. SIMBA SC — Mechi 19 — Pointi 42 (+25)

Leave a Comment