
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amempokea mgeni wake rasmi, Rais wa Jamhuri ya Kenya, William Ruto, katika viwanja vya Ikulu iliyopo jijini Dar es Salaam, leo Jumatatu, Mei 4, 2026, akiwa katika ziara ya kitaifa nchini Tanzania.
Ziara hiyo imejikita katika kuimarisha uhusiano wa kidiplomasia, kiuchumi na kijamii kati ya mataifa haya mawili jirani ya Afrika Mashariki.
Aidha, katika ziara yake hiyo, Rais Ruto anatarajiwa kulihutubia Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma kesho Jumanne, ambapo atazungumzia masuala mbalimbali ya ushirikiano wa kikanda na maendeleo ya pamoja.
