×

Video: Karen Aliyetoweka Arusha Adaiwa Kutuma Fedha Kutoka Nje ya Nchi, Dada Yake Afunguka – Video

Wasiwasi umeendelea kutanda jijini Arusha kufuatia kupotea kwa wasichana wawili, Karen Mark Didas (23) na Nakivona Toroka (22), ambao hawajaonekana kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Tukio hilo limeibua mjadala mkubwa kwenye mitandao ya kijamii huku familia, marafiki pamoja na wananchi wakitaka majibu ya haraka kutoka kwa vyombo vya usalama kuhusu hatima ya vijana hao.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na familia, Karen alionekana kwa mara ya mwisho Juni 21, 2025 baada ya kumweleza mmoja wa watu wake wa karibu kuwa alikuwa anaelekea Namanga kumsindikiza rafiki yake Nakivona kwenda kuonana na mpenzi wake.

Inaelezwa kuwa tangu siku hiyo, simu ya Karen haikupatikana tena hali iliyoongeza hofu na sintofahamu kwa ndugu na jamaa.

Akizungumzia tukio hilo, dada wa Karen amesema familia imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kuwatafuta wasichana hao huku ikiendelea kushirikiana na vyombo vya dola ili kupata taarifa zaidi kuhusu walipo.

Kutoweka kwa Karen na Nakivona kumeendelea kuzua maswali mengi miongoni mwa wananchi, hasa kutokana na muda mrefu kupita bila kupatikana kwa taarifa yoyote rasmi kuhusu walipo.

Ripoti kamili ya tukio hilo inapatikana kupitia Global TV.

Imeandaliwa na Mwandishi Msomi @Korumba_Lebabazi.

Leave a Comment