×

Lulu Diva na D Voice Waweka Wazi Penzi Lao Hadharani, Watangaza Mpango wa Ndoa

Msanii wa muziki na filamu Bongo, Lulu Diva akifanya yake na msanii wa singeli kutoka kundi la WCB Wasafi, D Voice.

Msanii wa muziki na filamu Bongo, Lulu Diva, usiku wa kuamkia leo Mei 8, 2026 ameibua gumzo kubwa mitandaoni baada ya kuweka wazi hisia zake kwa msanii wa singeli kutoka kundi la WCB Wasafi, D Voice, wakati wa uzinduzi wa duka lake jipya lililopo jijini Dar es Salaam.

Katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na mastaa mbalimbali nchini, Lulu Diva alionekana akimlisha D Voice keki mbele ya kadamnasi jambo lililozua shangwe na mjadala mkubwa miongoni mwa mashabiki wao.

Msanii wa muziki na filamu Bongo, Lulu Diva

Baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza, D Voice alimpongeza Lulu Diva kwa hatua aliyofikia ya kufungua biashara yake mpya, huku akieleza wazi kuwa anampenda sana. Aidha, alimtakia afya njema katika kipindi chake cha ujauzito na kumuombea ajifungue salama.

“Nampongeza sana mpenzi wangu Lulu Diva kwa hatua hii kubwa. Nampenda sana na namuombea ajifungue salama. Mungu ajalie yale yote tuliyopanga yaende sawa kuelekea kwenye ndoa yetu,” alisema D Voice.

Mbali na maneno hayo yaliyowavutia wengi, D Voice pia alieleza kuwa amemnulia Lulu Diva gauni lenye thamani ya shilingi milioni 1.5 kutoka kwenye duka hilo jipya kama sehemu ya kumuunga mkono katika biashara yake.

Tukio hilo limeendelea kuzua mijadala mitandaoni huku wengi wakivutiwa na namna wawili hao walivyooneshana mapenzi hadharani.

Msanii wa singeli kutoka kundi la WCB Wasafi, D Voice.

UNDANI wa USHAHIDI ULIOMTIA HATIANI ‘MR BLUE’ na KUHUKUMIWA KUNYONGWA kwa KUMUUA EZENIA KAMANA…

Leave a Comment