×

Rais Samia Aelekea Kigali Kushiriki Mkutano wa Nishati ya Nyuklia Afrika (NEISA 2026)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Mei 19, 2026 anaondoka nchini kuelekea Kigali, Rwanda, kushiriki Mkutano wa Uvumbuzi wa Nishati ya Nyuklia barani Afrika (NEISA 2026).

Mkutano huo utakutanisha viongozi wa Serikali, watunga sera, wawekezaji, wadhibiti na wadau wa sekta ya nishati kujadili nafasi ya nishati ya nyuklia katika kuimarisha usalama wa nishati, viwanda na maendeleo endelevu barani Afrika.

Mkutano wa NEISA 2026 unatoa nafasi kwa Tanzania kushiriki katika ajenda ya Afrika ya matumizi salama ya teknolojia ya nyuklia katika nishati, afya, kilimo, viwanda na utafiti.

Leave a Comment