
Kampuni inayojihusisha na shughuli za mauzo ndani ya maduka ya Shopers, City Mall pamoja na Aura imetangaza nafasi za kazi kwa wanawake wenye uwezo wa kufanya kazi za Customer Care pamoja na Shop Sales ndani ya jiji la Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa tangazo hilo, waombaji wanatakiwa kuwa smart na nadhifu, waaminifu pamoja na kuwa na uwezo mzuri wa mawasiliano kwa ajili ya kuhudumia wateja na kuongeza ufanisi wa mauzo ndani ya maduka hayo.
Waajiri wameeleza kuwa nafasi hizo zinawahusu wanawake pekee ambao ni wakazi wa Dar es Salaam, huku mshahara uliotajwa ukiwa ni Shilingi 350,000 kwa mwezi.
Waombaji wenye sifa wanatakiwa kuwasiliana kupitia WhatsApp pekee kwa namba +255 703 854 777 kwa ajili ya hatua zaidi za usaili na maelekezo ya kazi.