Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limethibitisha kuwakamata raia wa China wanne kwa tuhuma za kuwateka nyara raia wengine wawili wa taifa hilo.
Kwa mujibu wa taarifa ya polisi, watuhumiwa hao walitumia gari lenye namba za usajili bandia pamoja na mbinu mbalimbali kutekeleza tukio hilo la utekaji.