
Mfanyabiashara na mmiliki wa baa za Kitambaa Cheupe, Jesca Kikumbi ameibua mjadala mkubwa mitandaoni baada ya kuposti video kwenye Insta Stori yake akiwa pamoja na mfanyabiashara, Fred Ngajiro maarufu Fred Vunjabei huku akiambatanisha na maneno ya “My Man”, jambo lililozua maswali kwa mashabiki kuhusu ukaribu wao.
Video hiyo imekuja kipindi ambacho tayari kumekuwa na tetesi zikidai wawili hao huenda wakawa kwenye mahusiano ya kimapenzi, ingawa hakuna kati yao aliyewahi kuweka wazi kuhusu suala hilo.
Jesca ambaye amekuwa akijitambulisha kuwa yupo single baada ya kuachana na aliyekuwa mume wake, sasa ameonekana kuzidi kuwapa nafasi mashabiki kuendelea kuhusisha jina lake na Vunjabei kutokana na posti hiyo iliyosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii.
