
Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema bado kuna kazi kubwa ya kufanyika ili wananchi waweze kuliamini zaidi Jeshi la Polisi na kuliona kama sehemu salama ya kupata msaada wanapokumbana na changamoto mbalimbali.
Rais Samia amesema hayo baada ya kutazama video mtandaoni iliyokuwa ikielezea kiwango cha kukubalika kwa majeshi ya polisi barani Afrika miongoni mwa wananchi wake.
Akizungumza kuhusu taarifa hiyo, Rais Samia amesema nchi iliyoonekana kuongoza katika viwango vya kuaminiwa ilikuwa na asilimia 25 huku Tanzania ikitajwa kuwa na asilimia 12 pekee, hali ambayo imeonyesha umuhimu wa kuendelea kuboresha mahusiano kati ya Jeshi la Polisi na wananchi.
Amesisitiza kuwa ni muhimu kwa vyombo vya usalama kuhakikisha wananchi wanajenga imani navyo na kuviona kama sehemu ya msaada na ulinzi wakati wote wanapopata matatizo au wanapohitaji huduma za kiusalama.



