×

Marekani Yaionya Oman Kuhusu Ushuru Katika Mlango wa Bahari wa Hormuz

Waziri wa Fedha wa Marekani, Scott Bessent.

Waziri wa Fedha wa Marekani, Scott Bessent amesema Oman imeihakikishia Marekani kuwa haina mpango wa kuweka ushuru kwa meli zinazopita katika mlango wa bahari wa Hormuz.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Ikulu ya Marekani, Bessent alisema alizungumza moja kwa moja na balozi wa Oman kuhusu suala hilo na kusisitiza kuwa Marekani haitaruhusu mfumo wowote wa ushuru katika eneo hilo muhimu kwa biashara ya mafuta duniani.

“Ilikuwa wazi kuwa jambo hilo halikubaliki,” alisema Bessent huku akionya kuwa taasisi au watu watakaohusika kuweka au kusaidia ushuru huo wanaweza kuwekewa vikwazo vya Marekani.

Kauli hiyo imekuja baada ya Rais wa Marekani Donald Trump kuonekana kutoa onyo kali kwa Oman siku ya Jumatano alipoulizwa kuhusu uwezekano wa Oman na Iran kusimamia kwa pamoja njia hiyo ya baharini.

Marekani pia imesema itawawekea vikwazo watu au kampuni yoyote itakayolipa ada hizo kwa Iran, ikidai kuwa hatua hiyo inaweza kusaidia shughuli za kikosi cha Iran Revolutionary Guards.

Kwa sasa Iran imekuwa ikidhibiti kwa kiasi kikubwa usafiri katika mlango wa bahari wa Hormuz tangu kuanza kwa vita kati ya Marekani, Israel na Iran mwishoni mwa Februari mwaka huu.

Takribani asilimia 20 ya usambazaji wa nishati duniani hupitia katika njia hiyo ya bahari, hali ambayo imesababisha kupanda kwa bei za mafuta na mbolea duniani kutokana na usumbufu wa usafirishaji.

#PART2: JINSI POLISI WALIVYOHUKUMIWA KUNYONGWA kwa KUMUUA MFANYABIASHARA wa MADINI MTWARA….

Leave a Comment