
Waziri Mkuu wa Tanzania, Mwigulu Nchemba, amefanya mazungumzo na Balozi wa Palestina nchini Tanzania, Salam Abu Sharar, leo Jumanne Juni 2, 2026 katika Ofisi yake iliyopo Bungeni jijini Dodoma.
Mazungumzo hayo yamelenga kuendeleza na kuimarisha zaidi uhusiano wa kidiplomasia pamoja na ushirikiano kati ya Tanzania na Palestine katika sekta mbalimbali za kiuchumi, kijamii na maendeleo.

