×

Rais Samia Aweka Shada la Maua Kaburi la Askari Asiyejulikana Moscow

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan akiweka Shada la maua katika Kaburi la Askari Asiyejulikana (Tomb of the Unknown Soldier) pembezoni mwa Ukuta wa Ikulu ya Kremlin Jijini Moscow nchini Urusi tarehe 03 Juni, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameweka shada la maua katika Kaburi la Askari Asiyejulikana (Tomb of the Unknown Soldier) lililopo pembezoni mwa Ukuta wa Ikulu ya Kremlin jijini Moscow, Urusi, tarehe 03 Juni 2026.

Tukio hilo ni sehemu ya heshima maalum kwa mashujaa waliopoteza maisha yao vitani kwa ajili ya kulinda taifa la Urusi. Hafla hiyo ya kihistoria imehudhuriwa na viongozi mbalimbali pamoja na maafisa wa serikali ya Urusi.

Hatua hiyo pia inaashiria kuendelea kuimarika kwa mahusiano ya kidiplomasia na ushirikiano wa kihistoria kati ya Tanzania na Shirikisho la Urusi katika nyanja mbalimbali za maendeleo.

Leave a Comment